Wahamasishaji maarufu wa ujasiliamali Afrika Mashariki na Kati, Eric Shigongo na James James Mwang’amba wakiwasalimia umati kabla ya kuanza semina.
LET SHARE ................................
Uzinduzi huo ulifanyika kuanzia saa nane na nusu mchana katika huo ambapo Shigongo akiambatana na wajasiliamali, James Mwang’amba ambaye ni Mkurugenzi wa Mwang’amba Communication LTD pamoja na Dk. Didas Lunyungu, Mkurugenzi Mjasiriamali Kwanza Enterprises LTD ambao nao wanatoa elimu katika semina hiyo.
Katika uzinduzi huo Shigongo ndiye aliyeanza kuzungumza ,alianza kwa kuelezea historia ya maisha yake kwa ufupi huku akifafanua kuwa ni dhahiri kila mmoja sasa ni wakati wake kufanya mabadiliko katika kubadili maisha yake.
Alisema kuwa yeye ni mmoja wa watu waliotoka katika maisha ya umaskini, manyanyaso na hata kuitwa majina ya kuashiria hali ya maisha ya ufukara kwa kuitwa majina kama, Madaso akimaanisha mtu anayevaa nguo zilizochanika na akaamua mkoani Mwanza na kwenda jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kutafuta maisha huku akilala katika stendi ya daradala ya Kisutu Posta.
Alifafanua kuwa aliweza kutoka katika hali aliyokuwa nayo na sasa kuwa katika hali ya unafuu, hivyo sasa Tandale atatoa mafunzo katika semina hiyo ambayo yataweza kuwasaidia wakazi wa eneo hilo kutoka katika maisha waliyonayo na kuwa katika sehemu nyingine.
Alielezea namna maeneo hayo ya Tandale yanavyosahaulika hata katika mgao wa umeme ukilinganisha na Masaki e ,Masaki na hata maeneo mengine,hivyo sasa alisema sasa ni wakati mufaka kwa wananchi hao kujifunza siri ya utajiri.
Aliwaeleza jinsi alivyoanza kuandika vitabu vyake na kuviuza bila kusoma vya wengine kama njia mojawapo ya ujasiliamali.
Nao James Mwang’amba pamoja na Dk.Didas Lunyungu wote kwa pamoja waliweza kusalimiana na waliohudhuria semina hiyo na kutoa ufafanuzi kwa ufupi huku, wakielezea namna walivyojipanga katika kutoa mafunzo leo ambayo yatawatoa katika sehemu waliyopo na kuwa katika sehemu nyingine ya kimaendeleo.
Semina hiyo itaendelea leo katika uwanja huo kuanzia saa 8:30 mchana mpaka 12 jioni,na pia itakuwepo kesho mpaka siku ya mwisho ambayo itakuwa ni Jumamosi Aprili 4.
PICHA/STORI NA DENIS MTIMA/GPL
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni