Rais anayeondoka mamlakani nchini
Nigeria Goodluck Jonathan, amesema amesikitishwa kuwa siasa zilipewa
kipau mbele, kuliko maslahi ya wasichana waliotekwa nyara na kundi la
Boko Haram kutoka shule moja kwenye mji wa Chibok katika jimbo la Borno.
Msemaji wa kundi linalojiita Bring Back Our Girls (Aisha Yesufu) aliiambia BBC kuwa serikali ya rais Jonathan kwanza haikuamini kuwa wasichana hao walikuwa wametekwa.
Lakini rais Jonathan alikilaumu chama cha upinzai kinachosimamia jimbo na Borno kwa kusababisha mchanganyiko wakati wasichana hao walipotekwa.
Siku ya Jumatatu mkazi mmoja wa mji ulio kaskazini mashariki mwa nchi wa Gwoza alisema kuwa aliwaona baadhi ya wasichana hao wiki tatu zilizopita walipokuwa wakitoka kwenye nyumba moja kubwa karibu na nyumba yake.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni