wameamua kuwaajiri watoto wao waliomaliza kidato cha nne kufundisha Shule ya Msingi Visezi, ili kutatua tatizo la upungufu wa walimu shuleni hapo.
Wananchi hao wamesema wanawalipa watoto hao Sh. 15, 000 kwa wiki kama posho ya kujikimu.
Walisema wameamua kuajiri watoto wao baada ya kuona hakuna juhudi zozote zinazofanywa na serikali kutatua tatizo hilo.
Wakitoa kero zao mbele ya Mbunge wa Bagamoyo, ambaye pia ni Waziri
wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa, Mwenyekiti wa
kijiji hicho Hamisi Kiatala, alisema katika kipindi cha zaidi ya miaka
kumi kero ya upungufu wa walimu katika shule hiyo ya Visezi haijawahi
kutatuliwa na kwamba ina walimu watano wa kiume na mahitaji ya walimu
ni 11.
Kitala alisema serikali ya kijiji kwa kushirikiana na wanakijiji
walifikia hatua hiyo ya kuwaajiri watoto wao wapatao saba, baada ya
kuona hakuna jitihada zozote zinazofanywa na serikali za kuletewa
walimu. Alisema anashangaa kuona hakuna uwiano wa walimu kati ya kijiji
hicho na vijiji vya jirani na kufafanua kuwa Shule ya msingi Vigwaza
ina walimu 30 na Ruvu Darajani ina walimu 27.
Alisema mbali ya kero hiyo, wananchi wa kijiji hicho wanakabiliwa
na ukosefu wa maji ambayo si ya uhakika na katika vitongoji vitatu vya
Changedere, Kisogo na Chauru hawana huduma ya maji kabisa na hununua
ndoo moja Sh.700/= katika vijiji vya jirani.
Mkazi mwingine wa kijiji hicho Mashauri Tengeneza alimtaka mbunge
huyo kutatua kero hizo haraka na kumtishia kuwa asipotatua kabla ya
mwezi Oktoba CCM haitaweza kushinda kwani haijawafanyia kitu kwa
kipindi cha miaka kumi.
“Ngoja tukwambie, sisi wanavisezi wote ni wanaCCM kwa hiyo usiwe na
wasiwasi lakini kama hutatatua hizi kero zetu CCM itashinda kwa shida
sana, sio siri,” alisema.
Akijibu kero hizo, Kawambwa aliwataka wananchi hao kuwa na subira
na kuwa zile kero zinazowezekana atashughulikia kwa kushirikiana na
viongozi wa kijiji kabla ya mwezi Oktoba mwaka huu.
“Kero ya walimu itakwisha hivi karibuni kwani TAMISEMI wana mpango
wa kuwaajiri walimu, lakini viongozi wa kijiji hamjawahi kuniambia hizi
kero zenu wakati mimi ni mbunge wenu pia ndio waziri mwenye dhamana.
Ndugu wananchi hizi kero zinazowezekana kutatua nitazitatua kwa
kushirikiana na viongozi wa kijiji, zitakazoshindikana tutazishughulikia
mwakani kama nitarudi tena”, alisema.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni