hama cha rais mteule wa Nigeria APC, kimeshinda majimbo makuu ya Lagos Kaduna na Katsina katika uchaguzi mkuu wa Nigeria.
The All Progressives Congress (APC) ilihifadhi jimbo la Lagos mbali na kutwaa majimbo zaidi ya Kaduna na Katsina.
Ushindi huu wa majimbo zaidi unaiongezea pondo serikali mpya haswa baada ya kutwaa ushindi mkubwa dhidi ya Rais Goodluck Jonathan.
Matokeo kamili ya kura za majimbo 39 na magavana 29 unatarajiwa kutolewa baadaye.
Magavana 29 wa Nigeria wanaushawishi mkubwa kutokana na uwezo wao mkubwa wa kiuchumi
Lagos
Uchaguzi huu wa majimbo umeendeleza dhana ya kuwa APC itazoa maeneo wakilishi mengi kufuatia ushindi wa wa kihistoria wa jenerali mstaafu Muhammadu Buhari.
Siku ya jumapili, tume huru ya uchaguzi nchini humo (Inec) ilitangaza rasmi kuwa chama cha Jenerali mtaafu Buhari APC ilikuwa imetwaa jimbo la Lagos mbali na kushinda ugavana wa majimbo ya Kaduna na Katsina majimbo
ambayo yaliongozwa na kudhaniwa kuwa ni ngome ya PDP
Kwa wadadisi wengi utawala wa Jenerali mstaafu Buhari utakuwa utawala wa kwanza kutawala nchi na vilevile mji mkuu wa kiuchumi nchini humo wa Lagos tangu kumalizika kwa utawala wa kiimla mwaka wa 1999.
Vilevile hii ndio itakayokuwa mara ya kwanza kwa chama ambacho sio PDP kuwahi kuiongoza majimbo ya Kaskazini mwa taifa hilo.
Uongozi wa majimbo 36 unaumuhimu mkubwa haswa kiuchumi kwani magavana wengi katika maeneo yenye utajiri mkubwa wa mafuta huwa wana makadirio ya bajeti makubwa hata zaidi ya mataifa mengine ya Magharibi mwa Afrika.
Chama cha PDP hata hivyo kilihifadhi jimbo la Rivers
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni