Kwa mwaka mmoja unusu sasa , bi Annegret Raunigk ambaye ni mwalimu wa kingereza na kirusi amekuwa akijaribu kupata mtoto mwingine kwa njia ya upandikizaji,
Kulingana na vyombo vya habari vya German RTL.
Bibi huyo anasema kuwa alilazimika kuwatafuta watoto zaidi baada ya kitinda mimba wake mwenye umri wa miaka 9 kumsihi umtafutia watoto atakaocheza nao.
Bi Raunigk, ambaye amebeba mimba hiyo kwa majuma 21 sasa anasema kuwa alishtuka kujua kuwa alikuwa amejaaliwa mimba ya watoto 4 wala sio mmoja kama alivyotarajiwa.
Mwanamke mwenye umri wa miaka 65 mama ya watoto 13 sasa anamimba ya pacha wanne
Aidha mwanawe Leila alizua majadala mkali alipozaliwa mwaka wa 2005 lakini hilo halimsumbui bibi huyo ambaye miaka kumi ijayo atakuwa na tineja na watoto wachanga.
Mwanawe wa kwanza ana miaka 44.
Mahojiano ya bibi huyo na runinga hiyo ya kijerumani yanatarajiwa kuvutia hisia nyingi itakapopeperushwa baadaye leo.
Mbali na kufurahiwa wanawe 13 Bi Raunigk anawajukuu 7.
Mama mwenye umri wa miaka 65 Annegret Raunigk amejaliwa mimba ya pacha wanne
Kufikia sasa mwanamke anayeshikilia rekodi duniniani ya kuwa mama aliyejifungua pacha wanne ni Merryl Fudel,aliyejifungua akiwa na umri wa miaka 55.
Vilevile mwanamke ambaye anashikilia rekodi ya kujifungua akiwa na umri mkubwa zaidi ni Omkari Panwar, kutoka India aliyejifungua akiwa na miaka 70.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni