Wakimbizi wa Somalia katika kambi ya wakimbizi wa Daadab nchini Kenya
Serikali ya Kenya imeupatia Umoja wa
Mataifa makataa ya miezi mitatu kuwahamisha wakimbizi wa Somalia
wapatao nusu milioni hadi nchini Somalia.
Naibu rais William Ruto
amesema kuwa iwapo Umoja wa mataifa utakataa kuwahamisha wakimbizi hao,
Kenya itachukua jukumu la kuwandoa.Makataa hayo yanajiri siku kadhaa baada ya shambulizi la chuo kikuu cha Garissa ambapo takriban watu 148 waliuawa na kundi la wapiganaji wa Al-shaabab.
Baadhi ya wakimbizi wamekuwa wakiishi katika kambi za Dadaab mashariki ya taifa hilo kwa zaidi ya miongo miwili.
Kenya imelishtumu kundi la Alshabaab kwa kujificha katika kambi hizo huku likiwasajili wanachama wapya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni