Mbunge wa zamani wa Jimbo la Korogwe Vijijini, Mussa Lupatu ni miongoni mwa waliofariki katika ajali ya basi kijiji cha Mbwewe, Mkata wilayani hapa.
Kwa mujibu wa Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki,
Lupatu alipata ajali hiyo akitokea Kibaha kuelekea Korogwe kumpeleka
mwanae, Idrisa Lupatu, ambaye naye ni marehemu kupatiwa matibabu ya
ugonjwa wa akili.
Wengine waliyotajwa kufariki katika ajali hiyo ni karani wa
Mahakama ya Ardhi Dar es Salaam, Devota Msimbe, aliyefariki akikimbizwa
Hospitali ya Muhimbili.
Wengine waliotambuliwa ni Secilia Temba na watoto wake wawili,
Wilfred Temba na Heppnes Temba, akiwamo dereva wa basi la Ngorika, Abas
Mwamsele na Marry Serango, wakazi wa Moshi mkoani Kilimanjaro.
Aidha, Ndaki alisema maiti tatu hazijatambuliwa na miili yao imehifadhiwa katika hospitali ya magunga wilaya Korogwe.
Aidha, majeruhi 12 kati ya 34 wamelazwa katika hospitali tofauti,
wakiwamo saba waliopelekwa Muhimbili, mmoja hospitali ya wilaya ya
Handeni na wanne kituo cha afya Mkata, wilayani Handeni.
MUHIMBILI
Waliyolazwa Muhimbili ni Suli Murutu (46) mkazi wa Chanika, Dar es
Salaam, Said Salum (35), dereva wa basi la Ratco, Mohamed Bashiri (23),
mkazi wa Dar es Salaam, Augustino Lupatu, mkazi wa Kihaba, Mohamed Abdul
na wawili waliotambuliwa kwa jina moja la Boazi na Soshi.
HANDENI
Majeruhi waliolazwa katika hospitali ya wilaya ni Bakari Mbonea,
mkazi wa Handeni wakati waliopo kituo cha afya Mkata ni Joseph Mafita
(46), mkazi wa Dar es Salaam, Bilhud Hamisi (61), mkazi wa Moshi, Moris
Daniel (34), mkazi wa Dar es Salaam na mtoto wa miezi minane,
Giftclisantus Temba, ambaye hata hivyo amekabidhiwa kwa baba yake kwa
uangalizi zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni