Wanaume wengi wenye umri kati ya miaka arobaini na 50 wamo katika hatari kubwa ya kujiua kuliko wanawake.
Kijana
mmoja kutoka Uingereza ,Simon Jack alifanya utafiti huo baada ya baba
yake kujiua katika siku yake ya kuzaliwa miaka 25 iliyopita akiwa na
umri wa miaka 44.Jack anasema alianza kuwa mdadisi kwa simulizi zote au habari kuhusu watu wanaojiua na amegundua kuwa wote ni wanaume.
Idadi hiyo imekuwa kubwa zaidi kuliko wakati wowote katika miaka 14 iliyopita ya wanaume wanaomaliza maisha yao wenyewe ni mara nne ya wanawake.
Jack,alitamani kufahamu sababu inayowafanya wanaume kufanya matukio hayo zaidi.
Na kama kuna namna yeyote ya kuzuia mauaji haya, ''Nilijiuliza nini kinachopelekea wanaume hawa kufanya hivi?
''Au sababu yoyote ambayo inaweza kumpa shinikizo mwanaume ambaye anahitajika kuhudumia familia yake''.
Kwa upande wa baba yake Jack, haikuwa hivyo kwani alikuwa ni baba mzuri mwenye upendo kwa familia yake,mwenye uwezo nau maarufu.
Wengine walitoa maoni kuwa wengi wanaojiua ni ushahidi tosha kuwa wana matatizo ya kiakili au wana msongo wa mawazo au huzuni katika maisha.
Prof Rory O'Connor ambaye anaongoza kituo maarufu duniani cha utafiti katika chuo kikuu cha Glasgow,
anasema tabia ya kujuiua ni tatizo la kisaikolojia ambalo hutokana na upungufu wa kiakili.
Hata hivyo katika maamuzi kuna tofauti kubwa kati ya namna wanaume na wanawake wanavyo weza kujielezea matatizo yao na kuyatatua.
''wanawake huwa wanatumia njia za kujieleza ambazo ni rahisi watu kumuokoa tofauti na wanaume''
Jack anasema ”Natamani kujua nini kilimpata baba yangu kwani fumbo hili linaweza jibu maswali ya familia nyingi wenye matatizo kama yangu”.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni