MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Alhamisi, 23 Aprili 2015

Pepo la ajali lagubika nchi.

                      basi la unique na lori baada ya kupata ajari
Pepo la ajali limeigubika nchi baada ya watu 10 kufariki katika  ajali mkoani Shinyanga na kufikisha idadi ya watu waliokufa kwa ajali  katika kipindi cha wiki mbili kufikia 59.


miili ya watu waliopoteza maisha katika ajari 

Pepo la ajali za barabarani lilianza Aprili 10, mwaka huu hadi jana na kusababisha vifo hivyo na mamia ya watu kujeruhiwa katika mikoa kadhaa nchini. Katika ajali ya jana, watu tisa walifariki dunia papo hapo na mmoja akifia hospitalini baada ya basi walilokuwa wakisafiria kutoka jijini Mwanza kwenda Tabora kugongana na tela la lori la kampuni ya Coca - Cola katika kijiji cha Samuye, Shinyanga Vijijini.

 
Ajali hiyo ilitokea jana saa 8:45 mchana katika kijiji hicho, baada ya basi la kampuni ya Unique namba T148 BKK aina ya Scania kukutana uso kwa uso na tela hilo lenye namba T635 AJT katika barabara kuu ya Shinyanga - Nzega.

Akizungumzakutoka eneo la tukio jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Justus Kamugisha, alisema ajali hiyo ilitokana na lori la kampuni ya Coca - Cola lililokuwa na tela kulipita gari lingine, lakini kabla tela halijaingia katika barabara yake, lilikutana na basi hilo lililokuwa katika mwendo kasi na kusababisha ajali hiyo.
 
“Ni watu 10 waliopoteza maisha katika ajali hiyo, lakini wengine 51 wamejeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga kupatiwa matibabu,” alisema Kamanda Kamugisha.
 
Hata hivyo, Kamanda Kamugisha alisema majina ya waliopoteza maisha kutokana na ajali hiyo yatatangazwa baadaye pamoja na majeruhi.
 
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Mkoa wa Shinyanga, Dk. Salum Mfaume, alithibitisha kupokea miili tisa huku mtu mmoja akifariki dunia hospitalini hapo wakati akipatiwa matibabu pamoja na majeruhi 51.
 
“Kweli tumepokea miili tisa ya watu waliokufa katika ajali, lakini mtu wa 10 alifariki dunia wakati akipatiwa matibabu, pia tuna majeruhi wengine 51 walionusurika kutokana na ajali ya basi hilo,” alisema Dk. Mfaume.
 
MFULULIZO WA AJALI
Aprili 10, 2015, watu 12 walifariki dunia katika ajali iliyohusisha mabasi matatu na gari dogo iliyotokea katika eneo la Mbwewe, Handeni, mkoani Tanga na Kikwaza, wilayani Mikumi, Morogoro. 
 
Aprili 12, 2015, watu 18 waliteketea kwa moto baada ya basi la Kampuni ya Nganga kugongana na lori katika kijiji cha Msimba, Mikumi kwenye barabara kuu ya Morogoro – Iringa.
 
Aprili 17, 2015, watu 19 walifariki dunia baada ya basi dogo la abiria Toyota Hiace kupinduka na kutumbukia mtoni katika eneo la Kiwira, wilayani Rungwe, Mbeya.
 
                       NA DANIEL MKATE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni