Kiongozi wa cheo cha juu zaidi
anayeiunga mkono Urusi katika eneo linalothibitiwa na waasi mashariki
mwa Ukrain amesema kuwa usitishwaji wa mapigano ulioafikiwa mapema mwaka
huu na serikali hautadumu.
Bwana Zakharchenko aliongeza kuwa kile angependa kuona ni kupanuka zaidi kwa eneo hilo.
Chini ya makubaliano ya Minsk ambayo yaliungwa mkono na Urusi , Ujerumani na Ufaransa , serikali ya Ukrain ungerejesha mipaka chini ya udhibiti wake.
Mapigano yameendelea licha ya kuwepo kwa makubaliano hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni