MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumatatu, 13 Aprili 2015

Miliband asema yuko tayari kuongoza

Ed Miliband kiongozi wa chama cha Labour nchini Uingereza

Kiongozi wa chama cha upinzani cha Labour nchini Uingereza, Ed Miliband amesema chama cha Labour kitabadili namna nchi inavyoendeshwa na nani wa kuiendesha."
Miliband amesema hayo wakati akizindua ilani ya uchaguzi ya chama hicho.
Amesema amepimwa
 kama kiongozi wa upinzani na yuko tayari kwa wadhifa huo, Bwana Miliband amesema chama cha Labour kitakuwa "chama cha mabadiliko na uwajibikaji".

Amekataa "orodha ya mapendekezo", yakihakikisha kuwa sera zote hazitahitaji ukopaji wa ziada.

Lakini waziri mkuu David Cameron amemshutumu Bwana Miliband kwa kujaribu "kuuhadaa" umma.
                         David Cameron waziri mkuu wa Uingereza
Ilani hiyo yenye kurasa 86 ambayo ina urefu wa maneno 20,421, inabainisha ahadi kuu za sera za chama cha Labour ambazo ni pamoja na:

■Kupandisha kima cha chini cha mishahara kufikia zaidi ya pauni 8 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2019 ■Kutopandisha nauli za usafiri wa treni kwa mwaka mmoja, unaogharimu pauni milioni 200, zinazolipwa kwa kuchelewesha uboreshaji wa barabara za malori za A27 na A358 ■Huduma ya watoto ya saa ishirini na tano kwa wazazi wenye watoto wa umri wa miaka mitatu na minne na haki mpya ya msaada wa kabla na baada ya shule, kulipiwa kutokana na kupanda kwa kodi ya mabenki ■Kutopandisha ankara za gesi na umeme hadi mwaka 2017, kwa hiyo zinaweza kuendelea kushuka na sio kupanda ■Pauni bilioni 2.5 kwa ajili ya mfuko wa huduma za afya wa NHS uliolipiwa kwa kiasi kikubwa na kodi za majengo yanayozidi thamani ya pauni milioni 2 ■Kuondoa malipo ya nishati wakati wa baridi kali kwa wastaafu matajiri wenye pensheni kubwa, kuweka kikomo cha marupurupu kwa watoto kinachoongezeka na kulinda malipo ya kodi. ■Punguzo la malipo ya masomo katika vyuo vikuu kutoka pauni 9,000 hadi 6,000
                             Jengo la bunge la Uingereza
Akizungumza huko Manchester,Bwana Miliband amesema ukurasa wa kwanza wa ilani ya chama cha Labour "inaweka ahadi ya kulinda fedha za taifa letu; dhamira ya wazi kwamba kila sera... inatimizwa bila kuongeza hata senti moja ya kukopa".

Labour haitaahidi kitu chochote ambacho haitaweza kutimiza, amesema, akilinganisha na chama tawala cha Conservatives ambacho amekielezea kama "chama cha matumizi ambayo hayaongezi chochote na ahadi ambazo hazitekelezeki".

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni