NI wikiendi nyingine tunakutana katika eneo letu la kupata darasa huru la uhusiano. Bila shaka mpenzi msomaji uko vizuri na unaendelea na maisha kama kawaida, karibu! mada yenye kichwa cha habari kilichopo hapo juu. je? kuna umuhimu wowote wanandoa kufichana vipato vyao.
Kuna tabia za wanawake ambao wanaficha mapato yao ili wayatumie katika vitu vyao binafsi na suala la matumizi yote ya nyumbani anamwachia mumewe.
TUENDELEE PALE TULIPOISHIA...
TUENDELEE PALE TULIPOISHIA...
Wanataka mume ndiyo atoe mahitaji yote ya nyumbani, yeye abaki na mshahara wake kwa matumizi anayoyajua mwenyewe.Mwanamke huyo hataki mumewe ajue anaingiza shilingi ngapi na kuanza kupanga matumizi. Kipato chake yeye anakitumia kwa mambo yake binafsi likiwemo suala la urembo wa mwili wake, gharama za kubadilisha nywele saluni na kujinunulia nguo mpya.
Vyote ndivyo vitu anavyovinunua kwa fedha zake binafsi na kwa matumizi yake binafsi. Yupo radhi ajinunulie nguo zake lakini watoto amuombe ‘mzee’ fedha ili akawanunulie nguo. Hilo ndilo kundi la wanaume na wanawake wabinafsi.
NINI CHA KUFANYA?
Ili kujua nini kinapaswa kufanyika kwa wanandoa, ni vyema tukalitazama kundi la pili kabla hatujasonga mbele. Kundi la pili ni la wanandoa ambao wanapenda kushirikisha kila kitu hususan suala zima la kipato.Wanafanya hivyo wakiwa wanaamini kwamba wao ni mwili mmoja hivyo wakiunganisha nguvu kwa kuelezana ukweli juu ya kipato chao, watapata suluhu ya pamoja na kuweza kupiga hatua.
Ili kujua nini kinapaswa kufanyika kwa wanandoa, ni vyema tukalitazama kundi la pili kabla hatujasonga mbele. Kundi la pili ni la wanandoa ambao wanapenda kushirikisha kila kitu hususan suala zima la kipato.Wanafanya hivyo wakiwa wanaamini kwamba wao ni mwili mmoja hivyo wakiunganisha nguvu kwa kuelezana ukweli juu ya kipato chao, watapata suluhu ya pamoja na kuweza kupiga hatua.
Wanaamini kwamba, kutokana na kiapo walichoamua kukiapa iwe ni kanisani au msikitini wakati walipokuwa wanaoana, wao ni kitu kimoja. Hawaoni sababu ya kufichana kwa sababu mwisho wa siku wote wanategemeana katika maisha yao yote ya duniani hadi pale mmoja wao atakapotangulia mbele ya haki.
Wanaona kuelezana kipato chao husaidia kupanga bajeti yao vizuri. Kama pato lao ni dogo na halikidhi mahitaji yao basi rahisi kutafuta njia mbadala ya kuweza kujiongezea kipato. Ni rahisi pia kwao kupanga njia sahihi ya matumizi itakayowafanya wavuke katika safari yao waliyoikusudia kuifikia.
Vitabu mbalimbali vya dini vinatufundisha kwamba, pindi mwanamke na mwanaume wanapofikia hatua ya kufunga ndoa, licha ya kuwa ni watu wawili, mnakuwa mwili mmoja, nafsi ni mbili lakini mnakuwa kitu kimoja katika maamuzi ya kila kitu ndani ya familia yenu.
Mnakuwa kitu kimoja kwa maana kwamba mwenzako ndiyo mtu wako wa karibu, ndiyo msiri wako. Ndiye anayekujua zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Ndiye ambaye anaweza kukupa msaada kabla ya mtu mwingine yeyote kukufikia.
Hapo ndipo Mungu alipofundisha kwamba kama mtu mnashirikiana kwa kila kitu basi hakuna shaka mkawa mwili mmoja hata kama nafsi ni tofauti. Muunganiko wenu wa kiroho ndio unaokamilisha maana ya mwili mmoja kwa Mungu.
Hapo ndipo Mungu alipofundisha kwamba kama mtu mnashirikiana kwa kila kitu basi hakuna shaka mkawa mwili mmoja hata kama nafsi ni tofauti. Muunganiko wenu wa kiroho ndio unaokamilisha maana ya mwili mmoja kwa Mungu.
Mke analazimika kumueleza kila kitu kinachomhusu na mume vivyo hivyo. Haijalishi litakuwa ni jambo la msingi au liwe ni la kawaida, wanandoa wanapaswa kushirikishana tu. Jambo laweza kuwa ni la kufurahisha, halina kichwa wala miguu lakini kwa kuwa ni mwili mmoja, bado wanalazimika kushirikishana.
Elezaneni ukweli juu ya vipato vyenu ili iwe rahisi kupanga bajeti yenu. Mume mueleze mkeo kipato chako na mke pia hapaswi kuficha kipato chake. Jadilini matumizi ya vipato vyenu pamoja. Mnapoweka pamoja vipato vyenu, linalofuata ni namna ya kuvitumia kulingana na mahitaji.
Kama ni suala la kusaidia wazazi wa pande zote mbili, mtaweka utaratibu mzuri wa kuwasaidia kwani pato lenu wote wawili mnalijua. Haikatazwi kuwa na vibiashara vidogovidogo au posho ya pembeni lakini vipato ni vyema mkavikusanya pamoja na kupanga matumizi pamoja.Mkizingatia hayo hakika mtaishi kwenye ndoa kwa raha mustarehe pasipokuwa na migongano ya kila kukicha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni