Polisi nchini Burundi wamerusha
mabomu ya kutoa machozi na maji, ili kuwatawanya mamia ya waandamanaji
katika mji mkuu Bujumbura.
Mwaandishi wa BBC mjini Bujumbura, anasema kuwa malori makubwa yanayobeba vitoa machozi yamewekwa tayari kukabiliana na waandamanaji hao kote katika mji huo.
Anasema kuwa wazazi wamekimbia shuleni ili kuwaondosha watoto wao na kuwapeleka nyumbani.
Bwana Nkurunziza hajasema hadharani iwapo atawania kiti cha urais kwa muhula mwingine, lakini kuna tetesi kuwa ana mpango wa kufanya hivyo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni