Utafiti uliofanywa na Benki Kuu ya Dunia kwa robo ya kwanza ya mwaka kuhusu hali ya kiuchumi barani Afrika, umeonyesha kuwa Tanzania ni kati ya nchi barani humo ambazo bado zipo imara kiuchumi ndani ya kipindi hicho.
Hata hivyo, baadhi ya nchi zikiwamo zinazozalisha na kusafirisha
kwa wingi nje bidhaa ya mafuta, zinatarajia kuonja makali ya mdodoro wa
uchumi ndani ya mataifa hayo tangu kipindi hiki hadi mwaka ujao.
Matokeo ya utafiti huo kwa kipindi cha robo ya kwanza ya mwaka
2015, yaliyotolewa jana na taasisi hiyo ya fedha duniani kwa kurushwa
moja kwa moja kwa nchi zote zilizopo kusini mwa Jangwa la Sahara,
Tanzania ikiwamo , kutoka Washington DC, Marekani.
Akitoa taarifa hiyo, Mchumi kiongozi wa Benki ya Dunia (WB), kwa
upande wa Bara la Afrika, Punan Chuhan, alitaja nchi ambazo zinajimudu
kiuchumi mpaka sasa kuwa ni Ivory Coast, Tanzania na Msumbiji.
Alitaja baadhi ya sababu kwa nchi hizo hasa Tanzania kubaki katika
hali nzuri wakati nyingine zikiteseka, kuwa ni miundombinu imara na
utengemavu katika shuguli za uchimbaji wa madini.
Hata hivyo, huo wa kwanza kutolewa na benki hiyo ya dunia barani
humo kwa mwaka huu kulingana na utaratibu wake, inaonyesha kuwa hali ya
uchumi kwa ujumla barani humo imeshuka kutoka asilimia 4.5 mwaka
uliopita hadi asilimia 4 mwaka huu.
Na Isaya Kisimbilu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni