MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumamosi, 11 Aprili 2015

JK apokea Ripoti ya Uchunguzi Operesheni Tokomeza.

                        Rais Jakaya Kikwete.

Rais Jakaya Kikwete jana amepokea Ripoti ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza, katika hafla fupi iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.
 
Akipokea ripoti hiyo, Rais Kikwete ameishukuru Tume kwa kazi nzuri na kuongeza kuwa amefurahi kuwa suala zima la Operesheni Tokomeza limefikia mwisho wake.
 
Aidha, Rais alisema kuwa serikali itaisoma ripoti hiyo na katika kipindi cha wiki mbili itatoa maelezo ya jinsi itakavyoshughulikiwa.
 
Alipokea ripoti hiyo kutoka kwa Balozi Jaji (mstaafu) Hamisi Msumi,  Mwenyekiti wa Tume ambayo Rais Kikwete aliiteua Mei mosi, mwaka jana, na kuitaka ichunguze tuhuma mbalimbali za uvunjifu wa sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea za utekelezaji wa Operesheni Tokomeza.
 
Aidha,  aliipa Tume hiyo jukumu la kupendekeza hatua stahiki za kisheria za kuchukua dhidi ya watakaobainika kuhusika na uvunjifu huo. Vile vile, Rais aliiagiza Tume hiyo ishauri namna bora ya utekelezaji wa Operesheni kama hiyo hapo baadaye.
 
Rais Kikwete pia aliipa Tume hiyo Hadidu za Rejea sita ambazo pia ziliainishwa  katika Taarifa ya Serikali Namba 131 ya 2014. 
 
Hadidu hizo ni kuchunguza namna Operesheni Tokomeza ilivyotekelezwa; Ambazo ni kuchunguza iwapo maafisa waliotekeleza Operesheni Tomokeza walizingatia sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea walizopewa; 
 
kama maofisa waliotekeleza Operesheni Tokomeza, kuna watu waliokiuka sheria yoyote wakati wa kupendekeza hatua zinazostahili kuchukuliwa dhidi ya maafisa wa  (f) Kupendekeza mambo yanayopaswa kuzingatiwa wakati wa kupanga na kama walivunja sheria, kanuni, taratibu na hadidu rejea walizopewa.
 
Utekelezaji wa Operesheni Tokomeza na hatua zilizochukuliwa na maofisa wa Operesheni Tokomeza dhidi ya wakosaji hao na mali zao zilikuwa sahihi; Operesheni Tokomeza waliokiuka sheria, kanuni, taratibu na hadidu za rejea za Operesheni hiyo; na kutekeleza Operesheni nyingine kama hii, ili kuepuka malalamiko mengine yasitokee.
 
Jaji Msumi alimweleza Rais Kikwete kuwa Tume ilitembelea mikoa 20 na wilaya 38 na kupokea malalamiko mbali mbali kutoka kwa Viongozi wa Serikali wakiwamo mawaziri wanne waliojiuzulu, watekelezaji wa Operesheni; na walalamikaji/wahanga wa Operesheni.
 
Jaji Msumi alimweleza Rais Kikwete kuwa Ripoti ya Tume ina Juzuu kumi, ikiwamo muhtasari wa Taarifa ya Tume, Taarifa yenyewe ya Tume na Juzuu ya tatu hadi ya tisa ikiwa ni Mwenendo wa Ushahidi (Proceedings) ambapo Juzuu ya kumi ikiwa ni vielelezo vilivyotolewa na mashahidi.
 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni