Mwanamitindo Iman Abdulmajid
man
Abdulmajid aliishi nchini Marekani kama mhamiaji haramu.
Kulingana
na mtandao wa yahoo,mrembo huyo kutoka nchini Somalia ambaye ameolewa
na mwanamuziki David Bowie tangu mwaka 1992-aliingia nchini Marekani kwa
kuidanganya serikali kuhusu umri wake kwa kuwa alikuwa mdogo mno
kusafiri kutoka Kenya bila wazazi wake ambao hakuwa nao.
Iman:Nilidanganya
na kusema kuwa nilikuwa na umri wa miaka 19 ili kupata pasipoti kwa
kuwa bila hivyo ningelazimika kupata rukhsa kutoka kwa wazazi wangu na
wazazi wangu hawangeniruhusu mimi kwenda Marekani.
Mbali na
kuidanganya serikali hiyo mwanamitindo huyo mwenye umri wa miaka 59 pia
aliwadanganya wazazi wake kwa makusudi kuhusu kule aliko.
Iman
alitarajiwa kuwa chuo kikuu cha Nairobi wakati alipoelekea New York ,kwa
hivyo alidhani kwamba wazazi wake hawatagundua kule alikokwenda lakini
baada ya mda mfupi baba yake alimuona katika gazeti la Newsweek.
Akizungumza
na Gazeti la New York,Iman alisema:Ni Gazeti hilo analosoma baba yangu
na alipokuwa akisoma aliona picha yangu na maandishi kwamba ''ndiye
mwanamitindo mrembo kwa sasa''.
Nilivunja sheria lakini hakuna mtu ambaye anaweza kunishika hivi sasa, alijigamba mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 60.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni