MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumatano, 22 Aprili 2015

Urusi ina Majeshi Ukraine:Marekani

                          Rais Barack Obama wa Marekani
Marekani imeilaumu Urusi kwa kuweka mfumo kujihami na mashambulizi ya anga Mashariki mwa Ukraine,hali ambayo ni kinyume na makubaliano yaliyosainiwa mwezi Februari mwaka huu.
Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Marekani Bi. Marie Harf, amesema hatua ya majeshi ya Urusi kujenga mifumo ya ulinzi wa anga karibu na eneo la mapigano ni kinyume na makubaliano. 
Harf pia ameishutumu Urusi kwa kupeleka vikosi zaidi vya wanajeshi katika eneo hilo na kuendesha mafunzo kwa makundi yanayoipinga serikali. 
Hata hivyo Urusi haijajibu lolote kutokana na tuhuma hizo za Marekani,lakini awali Urusi iliwahi kukanusha kuwa haina vikosi vya majeshi ndani ya Ukraine.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni