Raia wa Yemen wakikatika Ghuba ya Aden kwa boti ndogo
Mashirika ya umoja wa mataifa yamesema kuwa mamia ya raia wa Yemen
wamevuka ghuba ya Aden kwa kutumia boti ndogo na kuingia nchini Somalia,
Djibouti na Somaliland wakikimbia mapigano nchini mwao.
Shirika la
umoja wa mataifa la UNHCR limesema kuwa linaangalia eneo zuri kwaajili
ya kuweka kambi ya wakimbizi kwaajili ya raia hao.
Wakati huo huo
wakimbizi kutoka nchini Somalia bado wanaendelea kuingia nchini Yemen
kuepuka njaa na machafuko nchini mwao.
Shirika hilo la UNHCR linasema
kuwa Yemen inawahifadhi wakimbizi wapatao 238,000 kutoka Somalia.
Mwandishi wa BBC Africa Mary Harper anasema wazo la Yemen kufikiria kuwa
na kambi za wakimbizi nchini Somalia si la kawaida kwa kuwa ni kawaida
kwa raia nchini humo kuikimbia nchi yao kutokana na machafuko ya mara
kwa mara hali ambayo haiwezi kuwa eneo zuri kwa wakimbizi kuhifadhiwa.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni