Mawaziri wa mambo ya naje wa mataifa
sita makubwa duniani pamoja na Iran wakijadili mpango wa nyuklia wa Iran
mjini Lausanne, Uswis
Kwa mujibu wa mkataba huo, Iran itapunguza uwezo wake wa kurutubisha
madini ya urani huku ikiahidiwa kuondolewa vikwazo kwa awamu.
Rais Barack Obama amesema ni "uelewano wa kihistoria" uliofikiwa na Iran.
Mataifa makubwa ya dunia na Iran sasa yanalenga kuandika mkataba kabambe ifikapo Juni 30.
Muundo wa mkataba ulitangazwa na Umoja wa Ulaya na Iran baada ya siku nane za majadiliano mjini Lausanne.
Mazungumzo
kati ya mataifa makubwa matano jumlisha moja yaani-Marekani, Uingereza,
Ufaransa, China na Urusi pamoja na Ujerumani- na Iran katika mkutano
uliofanyika mjini Lausanne, uliendelea na kupitiliza muda uliopangwa wa
kufikia tarehe 31 Machi.
Mwandishi wa BBC kutoka mjini Lausanne,
Barbara Plett Usher, anasema baada ya kupitiliza muda uliopangwa na siku
mbili za majadiliano ya kina kati ya Iran na mataifa sita makubwa
duniani wameelezea muundo wao uliofikiwa katika mkutano huo kama
mafanikio makubwa.
Mkuu wa sera ya nje ya EU Federica Mogherini
Mwanadiplomasia wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya,Federica Mogherini,
alisoma taarifa ya pamoja ikielezea vipengele vikuu, ambavyo ni
kupunguza vinu vya uchakataji wa fito za nyuklia, kubadili zana za
kutengenezea nyuklia na ahadi ya kuondolewa vikwazo vya kimataifa dhidi
ya Iran.
Makubaliano yaliyofikiwa katika mkutano huo si ya maandishi, sio rasmi, bali yanajenga msingi wa kufanyika mazungumzo ya kina.
Lakini waanzilishi wa mazungumzo haya wanasherehekea mafanikio makubwa yaliyofikiwa, ambayo wanasema ni ya kihistoria.
Iran
imekuwa ikikana madai ya mataifa ya magharibi kuwa mpango wake wa
nyuklia unalenga kutengeneza silaha za nyuklia. Iran imeingia katika
mazungumzo haya ili kuona inaondolewa vikwazo.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani,
John Kerry na mwenzake wa Iran Javad Zarif katika mkutano wa mpango wa
nyuklia mjini Lausanne.
Mkuu wa sera ya nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini ametangaza
mkataba huo katika mkutano na waandishi wa habari akiwa pamoja na waziri
wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif, akisema hiyo ni "hatua ya maamuzi"
iliyofikiwa.
Waziri mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu
Kwa upande wake Rais Obama amemwambia Bwana Netanyahu kwamba mkataba
huo kwa namna yoyote ile unaondoa wasiwasi kwao kuwa Iran ni kinara wa
kufadhili ugaidi na vitisho dhidi ya Israel.
Mkataba huo pia
umekosolewa na wajumbe wa baraza la Congress la Marekani ambao wanataka
wabunge wa Marekani kuwa na haki ya kupitia kila makubalino ya mwisho
yanayofikiwa katika mkataba huo.
Nao wananchi wa Iran wanaoishi nchini Uswisi wameelezea kufurahishwa na mpango huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni