MMILIKI WA BLOG HII
Ijumaa, 3 Aprili 2015
GWT KUNOGESHA MTOKO WA PASAKA
KIKUNDI cha kusifu na kuabudu cha Glorious Worship Team (GWT), kinatarajia kunogesha mtoko wa Sikukuu ya Pasaka kwa kuwakutanisha watu mbalimbali kumuabudu Mungu kwa njia ya kuimba huku wakisherehekea kwa pamoja sikukuu hiyo sanjari na kupata semina ya mbinu za kutoka kuwa mwajiriwa hadi mwajiri ambazo zitatolewa na mhamasishaji mashahuri nchini, Eric Shigongo.
Mwenyekiti wa GWT, Emmanuel Mabisa aliliambia Ijumaa kuwa, Jumapili hii ya Pasaka, watasherehekea kwa namna tofauti hivyo watu wahudhurie kwa wingi katika ukumbi uliopo katika kituo cha mafuta cha Victoria jijini Dar.
“Huduma hii ni muendelezo wa huduma tuliyoianza Jumapili iliyopita, kila Jumapili tutakuwa pale kuimba, kuabudu na kupata semina kutoka kwa Shigongo. Niwasihi watu wote wahudhurie kwa kuanzia saa 9:00 alasiri mara baada ya ibada mbalimbali zitolewazo, tutakuwa pale kuhakikisha Neno la Mungu linawafikia kwa njia ya nyimbo zetu nzuri,” alisema Mabisa.
Mbali na huduma ya kuimba na semina ya Shigongo itakayotolewa bure, watakaofika siku hiyo watapata kusikia maneno kutoka kwa mshereheshaji mashuhuri Bongo, MC Pilipili.Aidha, Calvary Band na makundi mbalimbali ya waimbaji yatakuwepo kutoa burudani.
Stori: Musa Mateja
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni