Mratibu wa huduma za kibinadamu wa Umoja wa Mataifa nchini iraq amesema kuwa huenda takriban watu 40,000 wameukimbia mji wa Ramadi ambao ulitekwa na wanamgambo wa islamic state karibu wiki moja iliyopita.
Anasema kuwa kuna ripoti kwamba baadhi ya watoto wameaga dunia baada ya kuishiwa na maji mwilini.
Bwana Bartsch pia anasema kuwa umoja wa mataifa una wasi wasi kuhusu hatma ya wakimbizi waliojikuta kati kati ya mapigano kati ya wanamgambo wa Islamic State na vikosi vya serikali.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni