Mwanaharakati David Ndung'u Wanjohi
wa Ol Kalau kaunti ya mkoa wa kati nchini Kenya amejifunga nyororo
katika chumba cha dharura cha hospitali kuu ya Kenyatta Jijini Nairobi
na kuanza mgomo wa kutokula ili kupinga kile alichokitaja kama ukosefu
wa vifaa vya kuwasaidia wagonjwa wengi wa ugonjwa wa saratani nchini.
David ambaye ni baba wa watoto wawili amesema kuwa serikali na jamii kwa
jumla inapaswa kutoa raslimali zilizopo kununua vifaa vya tiba kwa
wagonjwa ambao wanangojea tiba hadi mwaka 2017.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni