Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa
SERIKALI imewataka wananchi kutoa maoni yatakayoiboresha sheria ya
makosa ya mitandao ya mwaka 2015 iliyosainiwa hivi karibuni na Rais
Jakaya Kikwete ili yasaidie kuiboresha.
Imesema licha ya sheria hiyo kusainiwa na Rais, bado kuna umuhimu wa kuiboresha katika baadhi ya vipengele vyenye upungufu.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa
Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, katika
mkutano wake na waandishi wa habari uliofanyika ofisini.
Mkutano huo uliandaliwa maalumu kwa ajili ya kuufahamisha umma kuhusu
kusainiwa kwa sheria hiyo na rais na kuelezea umuhimu wake, huku pia
waziri huyo akiitumia fursa hiyo kukaribisha maoni ya wadau mbalimbali
kwa ajili ya kuiboresha.
tutayatafakari na tutayafanyia kazi,” alisema Mbarawa.
Waziri Mbarawa alisema Tanzania si nchi ya kwanza kupitisha sheria ya
aina hiyo kwa sababu ya uwepo wa maendeleo ya teknolojia ya mawasiliano
kulikosababisha kuongezeka kwa uhalifu wa mitandao.
“Sisi siyo wa kwanza, Nchi za Uingereza, India, Malaysia, Uganda,
Korea Kusini, Singapore, Mauritius, Afrika Kusini, Marekani na
nyinginezo tayari zina sheria ya aina hii na inasaidia kuwapa wananchi
haki wanapofanyiwa uhalifu wa mitandaoni,” alisema Profesa Mbarawa.
Sheria ya Makosa ya Mitandao ni moja ya sheria zilizokosolewa kwa
kiwango kikubwa na wadau wa habari pamoja na makundi mbalimbali ya
kijamii, kwa madai kuwa inalenga kubana uhuru wa vyombo vya habari
pamoja na kubinya uwanja mpana wa ukusanyaji na utoaji habari kwa
waandishi wa habari.
Na Jonas Mushi,
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni