Wakati kukiripotiwa mvua kubwa na
tetemeko kubwa na jipya nchini Nepal, Wakuu nchini humo wamethibitisha
kuwa idadi ya watu waliokufa kutokana na tetemeko hilo jipya , imepanda
na kufikia zaidi ya watu 40.
Wakati huo huo helkopta ya kikosi cha
majini ya Marekani,ambayo ilikuwa ikifanya kazi ya kusaidia kusambaza
huduma za kibinaadamu nchini Nepal, haijulikani.
Maofisa wa serikali wa Marekani wamesema kwamba helkopta hiyo ilikuwa maeneo ya jirani na kijiji cha Charikot, ambacho kiliharibiwa vibaya na tetemeko la ardhi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni