Serikali ya Burundi imewaagiza
waandamanaji katika mji mkuu wa Burundi Bujumbura kusitisha maandamano
yao dhidi ya hatua ya rais wa taifa hilo Pierre Nkurunziza kuwania
muhula wa tatu katika uchaguzi wa mwezi ujao.
Hakuna maandamano yanayoendelea leo kufuatia vifo vya waandamanaji wawili lakini waandalizi wake wamesema kuwa maandamano yataendelea siku ya jumapili.
Takriban watu 18 wameuawa tangu maandamano hayo yaanze wiki mbili zilizopita.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni