Misa ya kuwatawaza watawa 2 wapalestina katika ukumbi wa st Peters Basilica huko Vatican
Hatua hii inatazamwa na wengi kama chambo cha kuwavutia wakristu katika maeneo ya mashariki ya kati ambapo wakristu wanahujumiwa na jamii.
Papa Francis amewatawaza watawa 2 wapalestina
Hapo jana Papa Francis alifanya mazungumzo na rais wa wapalestina Mahmoud Abbas katika makao makuu ya Vatican.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alimtunuku Abbas medali ya Amani huku akimtaja kuwa ''malaika wa amani''
Huduma ya mtakatifu Marie Alphonsine Ghattas - aliyezaliwa katika familia ya kipalestina mjini Jerusalem
Watawa hao Marie Alphonsine Ghattas - aliyezaliwa katika familia ya kipalestina mjini Jerusalem alianzisha huduma ya watawa ya - Rosary Sisters, ambayo hadi wa leo inaendesha shule za chekechea na zile za msingi.
Makabiliano baina ya Israeli na Wapalestina yamesababisha wakritu kupungua mashariki ya kati
Bi Mariam anasemekana kuwa alitenda miujiza miongoni mwa jamii yake huku akitambuliwa kwa kuonekana na alama za ishara ya kusulubishwa kwa Yesu Kristo msalabani.
Wawili hao waliishi katika enzi ya Ottoman ambapo wanawake hawakuwa na semi katika hali halisi ya maisha lakini waliibuka kuwa mifano ya kuigwa licha ya kuishi maisha ya uchochole na magonjwa mengi.
Wawili hao vilevile wanadaiwa kuwa na mawasiliano na mamake Yesu Kristo Maria Mtakatifu.
Kutawazwa kwao kunatarajiwa kuweka msingi yao kutambuliwa kama watakatifu kutoka kwenye chimbuko la ukristu.
takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wakristo imedidimia kwa asili mia 2% katika eneo la Palestina na Israili.
Hii inatokana na umaarufu mkubwa wa Waislamu na Wayahudi ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wapigana na kuwalazimu wakristu kutorokea mataifa salama kuepuka vita.
CHANZO BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni