Waziri wa mambo ya nchi za nje wa
Marekani John Kerry,amesema kwamba amekuwa na mazungumzo ya kirafiki
kuhusiana na mzozo wa Ukraine pamoja na mambo mengine na mwenyeji wake
rais wa Urusi , Vladimir Putin, katika ghuba ya bahari ya shamu pwani ya
Sochi.
Kerry pia hakusita kuzungumzia masuala ya ziada ambayo yalijiri katika mazungumzo yao kwamba ni juu ya yanaoendelea baina ya Iran na Syria. Amesema kwamba ni muhimu kuzingatia makubaliano waliyofikia baina ya Marekani na Urusi wakati wakiangazia masuala mengine yanayo ikabili dunia.
Mapema kabla ya kuanza mazungumzo hayo, waziri huyo ma mambo ya nchi za nje wa Marekani, alipata fursa ya kuweka shada la maua katika makaburi ya askari waliopigana vita vikuu vya pili vya dunia mjini Sochi. Uhusiano baina ya Urusi na Marekani umeshuka kwa kasi baada ya Urusi kujihusisha harakati za krimea na kuwaunga mkono wapiganaji wa waasi walioko upande wa Mashariki mwa Ukraine.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni