Katiba Inayopendekezwa ambayo itapigiwa kura na wananchi Aprili 30, mwaka huu awali ilikuwa na Ibara 28 ambazo Tume ya Mabadiliko ya Katiba chini ya Jaji Joseph Sinde Warioba iliona zinafaa kuwemo lakini Bunge Maalum la Katiba chini ya Spika Samwel Sitta ikaona hazifai, hivyo kuzifuta.
Ibara zilizoondolewa zimeleta malalamiko kwa baadhi ya wananchi kwani zimeonekana zinafaa zikiwamo zinazowataka viongozi wa umma kutopokea zawadi kwa manufaa yao binafsi wala kufungua akaunti ya benki nje ya nchi pasipo sababu maalum.
Leo tunamalizia kuwaletea ibara hizo zilizoondolewa ili wewe mwananchi uone kama zilifaa kuwepo kwenye katiba yetu au la:
120.-(1) Bunge litatumia madaraka yake ya kutunga sheria kwa kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria ambao utawekwa saini na rais.
(2) Bila kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (3), Muswada wa Sheria unaweza kuandikwa na serikali, Kamati ya Bunge au kikundi cha wabunge.
(3) Wakati wa kuandaa Muswada wa Sheria kuhusu jambo lolote la Muungano, Serikali ya Jamhuri ya Muungano itahakikisha kwamba inawashirikisha wananchi kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo juu ya muswada huo.
(4) Muswada wa sheria utahesabiwa kuwa umepitishwa na bunge iwapo utaungwa mkono kwa kura za wabunge wasiopungua theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Tanganyika na wasiopungua theluthi mbili ya wabunge wote kutoka Zanzibar.
(5) Bila kuathiri masharti ya Ibara ndogo ya (4), bunge litatunga Kanuni za Kudumu zitakazoweka utaratibu wa-
(a) kuwasilisha, kujadili na kupitisha Muswada wa Sheria; na
(b) utekelezaji bora wa masharti ya ibara ndogo ya (3).
129.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii, wananchi watakuwa na haki ya kumwondoa mbunge wao madarakani, endapo mbunge atafanya moja wapo au zaidi ya mambo yafuatayo:
(a) kuunga mkono sera ambazo zinaenda kinyume na masilahi ya wapigakura au kinyume na masilahi ya taifa;
(b) kushindwa kuwasilisha au kutetea kwa dhati hoja zinazotokana na kero za wapigakura wake;
(c) kuacha kuishi au kuhamisha makazi yake kutoka eneo la Jimbo la Uchaguzi kwa zaidi ya miezi sita bila sababu za msingi; au
(d) mambo mengine yatakayoainishwa kwenye sheria ya nchi.
(2) Bunge litatunga sheria kuweka masharti ya kuendesha uchunguzi kwa mbunge atakayeshindwa kutekeleza majukumu yake kwa wapigakura wake na utaratibu wa kumwondoa katika ubunge.
146.-(1) Bila ya kuathiri masharti ya Katiba hii yanayolinda na kuhifadhi uhuru wa mawazo na majadiliano katika Bunge, ni marufuku kusema uongo bungeni na kwa sababu hiyo, mbunge anapozungumza ndani ya Bunge ana wajibu wa kuhakikisha kwamba anatoa kauli au maelezo kuhusu jambo au suala ambalo yeye mwenyewe anaamini kuwa ni la kweli na siyo jambo la kubuni au la kubahatisha.
(2) Mbunge anapokuwa akizungumza bungeni hatahesabika wala kutafsiriwa kuwa anasema uongo iwapo anafanya rejea ya habari kuhusu jambo lililotangazwa au lililoandikwa na vyombo vya habari au nyaraka nyingine yoyote ambayo chanzo chake kinafahamika au kitaelezwa na mbunge huyo.
231. Vyanzo vya mapato ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano vitakuwa:
(a) ushuru wa bidhaa;
(b) mapato yasiyo ya kodi yatokanayo na taasisi za Muungano;
(c) mchango kutoka kwa nchi washirika;
(d) mikopo kutoka ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano; na
(e) mapato mengine.
234. Serikali za nchi washirika zitakuwa na benki zitakazokuwa na jukumu la kutunza akaunti ya fedha za serikali ya nchi mshirika husika, kusimamia sera za kifedha na benki za biashara katika mamlaka zao.
242.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania itakayokuwa na jukumu la kusimamia masuala yote ya utumishi katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
(2) Bunge litatunga sheria itakayoweka masharti kuhusu muundo, majukumu na mambo mengine yanayohusu Tume ya Utumishi ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania.
244.-(1) Katika utekelezaji wa majukumu yake, Jeshi la Polisi la Jamhuri ya Muungano litazingatia-
(a) viwango vya juu vya kitaaluma na nidhamu miongoni mwa wafanyakazi wake;
(b) ulinzi na ukuzaji wa haki za binadamu;
(c) kanuni za uwazi na uwajibikaji; na
(d) kukuza uhusiano na jamii.
(2) Jeshi la Polisi, katika kutekeleza majukumu yake, litashirikiana na vyombo vinavyohusika na kupambana na uhalifu vya Nchi Washirika katika kufanya uchunguzi na kushughulikia makosa ya rushwa na ufisadi.
246. Mkuu wa Jeshi la Polisi atatekeleza kazi zake kwa uhuru, bila woga, upendeleo wala chuki na kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii na sheria za nchi.
247.-(1) Kutakuwa na Tume ya Utumishi wa Jeshi la Polisi itakayokuwa na jukumu la kusimamia utumishi wa Jeshi la Polisi Tanzania.
JIUNGE NA GLOBAL BREAKING NEWS
Comment
Hadithi za Shigongo
TOP MEMBERS WIKI HII
1 |
GLOBAL |
2 |
sumon azam |
3 |
espnwish |
4 |
Ben |
5 |
robert ludger nyagali |
6 |
aslam uddin |
7 |
onikkosta |
8 |
Samwel Lusana |
9 |
Suzaney Jackson |
10 |
chodatrex |
Forum
ONGEZEKO LA VITENDO VYA UKAHABA NCHINI TANZANIA BILA UDHIBITI WA MAMLAKA HUSIKA, JE UFANYWE UJASILIAMALI?
naleta mjadala huu kwenu, kuhusu ongezeko
la kutisha la vitendo vya ukahaba nchini kwetu, mbaya zaidi ni kwa
vijana wadogo na wengine ni wasomi na wenye uwezo wa kifedha, cha ajabu
mamlaka husika ni kama zimefumba macho na kuweka pamba masikioni na…
JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?
JE? WAYAJUA MADHARA YA UTABIRI WA MATUKIO
HAZARANI KATIKA USALAMA WA NCHI?NDOTO ZA URAISI katika kitu cha
kustaajabisha, na cha kushangaza, Utakubaliana na mimi kua kumeibuka
tabia ya watu na baadhi viongozi tena wengine wa nyazifa za uwaziri
KUTOA…
MIUNDO MBINU TANZANIA
Watanzania wenzangu, naomba nisaidiwe hili
jambo ambalo limekuwa sugu hapa nchi,kila ikifika kipindi cha uchaguzi
barabara zinaanza kuchimbwa hasa vijijini na maeneo ya nje ya miji,je,
hii ni aina nyingine ya rushwa au ninini?na kama ni aina…
OKWI ANAIGHARIMU SIMBA, VIONGOZI WAMUANGALIA KWA JICHO LA TATU
Hakuna haja tena ya kufichana, Okwi
anaifanya Simba kama timu ya bonanza!!Lakini ajue Simba imeshindwa
kuwavumilia kina Kwizera, Mbiyavanga, Gervais Kago, Ssentongo n.k
yawezekana hawa wote walikuwa wana viwango kuzidi Okwi wakati wanatua…
Tags: OkwiTETESI: BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI HILI HAPA
Katika hali ambayo haikutarajiwa, rais
Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri.
Mabadiliko hayo ambayo yatatangazwa kesho jioni yamewatupilia mbali
watuhumiwa wa ufisadi sambamba na wazembe katika utendaji. Waliotupwa…
Tags: SIASAPOLISI KUPAMBANA NA WANAHABARI, WAFUASI WA CHADEMA NANI ALAUMIWE?
Jeshi la Polisi likiwa na silaha pamoja na
mbwa, Septemba 18, mwaka huu limepambana na wafuasi wa Chadema na
wanahabari waliofika katika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar
kufuatilia tukio la Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe…
Tags: VURUGUKIU YA WATANZANIA NI IPI, SERIKALI MBILI AU TATU?
Kitendawili kilichopo katika taifa leo kwa
sasa ni juu ya serikali ngapi zinafaa kuelekea kupata Katiba Mpya,
Serikali mbili au Serikali tatu?TOA MAONI YAKO HAPA!
Tags: katiba, siasaJUAN MATA KUTUA MANCHESTER UNITED ATASIADIA KULETA MATOKEO BORA BAADA YA TIMU KUSUASUA?
Juan Mata anataraji kutua Manchester United akitokea klabu ya Chelsea ya…
TOP NEWS WEEK HII
Latest Activity
- Top News
- Everything
You need to be a member of Global Publishers to add comments!
Join Global Publishers