mtoto alibebwa ndani ya kisandu
Mtoto mmoja wa miaka minane
amesafirishwa hadi nchini Uhispania kutoka Morroco akiwa ndani ya
sanduku kwa mujibu wa maafisa wa polisi wa Uhispania.Wakati polisi walipolifungua sanduku hilo, mvulana huyo alikuwa katika hali mbaya sana.Mvulana huyo kutoka Ivory Coast sasa anahudumiwa na mamlaka ya Cueta.
Gazeti la Uhispania El Paris liliripoti kwamba msichana huyo wa miaka 19 hana uhusiano na mtoto huyo na kwamba alilipwa na babaake ili kubeba sanduku hilo.
Babaake mtoto huyo anaishi katika visiwa vya Conary na kwamba alitarajia kuonana na mwanawe kulingana na gazeti hilo.
Babaake baadaye aliripotiwa kumlipa raia huyo wa Morocco ambaye alimsafirisha mtoto huyo kupitia sanduku.
Msemaji wa polisi aliiambia Efe:''Alionekana kusita na kama ambaye hakutaka kupitia mpakani''.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni