Bob Hewitt.STAA wa zamani wa tennis, Bob Hewitt amehukumiwa kwenda jela miaka sita kwa kosa la ubakaji nchini Afrika Kusini.
Bob Hewitt enzi zake.
Hewitt alikutwa na hatia Mwezi Machi jijini Johannesburg kwa makosa
mawili la ubakaji na udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto wa kike.Akizungumza wakati wa kutolewa hukumu hiyo, mke wa Hewitt aliiomba mahakama kuonyesha huruma kwa mumewe huyo mwenye umri wa miaka 75.
Makosa hayo yalifanyika miaka ya 1980 na 1990 wakati staa huyo aliyezaliwa Australia alipokuwa akifanya kazi ya ukocha nchini Afrika Kusini.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni