Mmoja wa majeruhi katika shambulio hilo akitolewa eneo la tukio.
WATU watatu wameripotiwa kupoteza maisha huku wengine takribani 20
wakijeruhiwa baada ya mlipuko kutokea kwenye uwanja wa ndege wa
kimataifa mjini Kabul nchini Afghanistan leo.
Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa mlipuaji wa bomu hilo la
kujitolea muhanga alikuwa amelenga wanajeshi wa kimataifa nje ya lango
kuu la uwanja huo wa ndege.
Lango hilo hutumika na vikosi vya kijeshi vya kigeni. Kundi la
Taliban limethibitisha kuhusika na shambulio hilo katika taarifa yake
lililoituma kwa wanahabari.
Shambulizi hilo linafanyika ikiwa ni siku tatu baada ya mwanamgambo
mmoja wa Taliban kuwaua watu 14 wakiwemo raia tisa wa kigeni katika
hoteli moja mjini humo.
Chanzo: BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni