Mshindi wa uchaguzi mkuu nchini Nigeria Muhamadu Buhari ameapishwa kama rais mpya wa nchi hiyo.
picha za sherehe hizo na maelfu ya mashabiki na wafuasi wake walishangilia Jenerali huyo mtaafu alipokula kiapo cha kulinda nchi hiyo.
Kimataifa, Buhari pia anasemekana kuheshimiwa.
Yajulikana kwamba ni yeye na marehemu Nelson Mandela tu ndio Wafrika binafsi waloalikwa na Ikulu ya White House, Marekani, kuhudhuria sherehe za kutawazwa Barack Obama.
Kampeni ya Jenerali Buhari, ilitilia mkazo mambo kadha, miongoni mwake utawala bora, kufufua uchumi, maendeleo ya miundombinu,
umeme na nishati, kilimo, elimu, afya, ardhi na usafiri, kuwezeshwa wanawake, usalama, na ajira. Ingawaje, uwili wa nafsi yake bado unazusha masuala, je ni wa kijeshi au kidemomkrasi..
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni