Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) unasikitika kuwataarifu
abiria wa treni ya Deluxe ya kwenda Kigoma leo Mei 17, 2015 saa 2
usiku kuwa safari hiyo imeahirishwa hadi kesho Jumatatu Mei 18, 2015
saa 2 usiku.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo sababu za kuahirishwa zinatokana na ajali mbili mfululizo za treni za mizigo.
Ajali ya kwanza ilitokea asubuhi saa 1:30 maeneo ya Stesheni ya Ngeta
mkoa wa Pwani na ya pili saa 5 asubuhi maeneo ya Stesheni za
Kinguruwila na Morogoro!
Ajali hizo zimehusisha kuanguka kwa mabehewa manne ( Ngeta ) na
kuacha njia behewa moja (Kinguruwila )! Treni zote mbili zilikuwa
zikielekea bara!
Tayari wahandisi na mafundi wa TRL wako katika maeneo ya tukio
kwa ajili ya kazi ya kuyaondosha mabehewa yaliopata ajali na pia
kukarabati njia ili ifunguliwe haraka na kurejesha mawasiliano ya njia
ya reli katika hali ya kawaida.
Kutokana na uzito wa kazi hiyo ya ukarabati njia ndio sababu kuu iliyopelekea safari ya Deluxe iahirishwe hadi kesho usiku!
Wakati huo huo taarifa imeongeza kusema kuwa ajali hiyo imeathiri
urejeshaji wa vichwa viwili vya treni ya Jiji ambavyo havotoweza
kufika Dar kwa wakati na hivyo kesho huduma ya treni ya Jiji
haitokuwepo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni