TANZANIA KUTIBU MARADHI YA MOYO BILA KUFANYA UPASUAJI
Baadhi ya Waandishi wa habari
wakifanya kazi yao na kuelekezwa namna (Cath Lab) mtambo wa kufanya
uchunguzi na kuzibua mishipa ya damu inayopeleka damu kwenye moyo na pia
kuziba matundu ndani ya moyo bila kufungua kifua.
Katikati
ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt.
Hussein Kidanto akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Prof.
Jameel Alata ambaye ni Daktari Mwelekezi wa Magonjwa ya Watoto ambaye
ameongoza timu ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan
Cardiac Centre iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo
Muhimbili kwa siku tisa kuanzia tarehe 8 hadi 16 Mei, mwaka huu. Kulia
ni Sheikh Said Ahmed Abri ambaye ni Mwenyekiti Mtendaji wa Shirika
lisilo la Kiserikali la Kiislam la hapa nchini liitwayo Dhi Nureyn
Islamic Foundation na shirika hili ndilo lililoratibu timu hii ya
madaktari kuja kutoa huduma.
Baadhi
ya madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre
iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia wakimsikiliza Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati akiwakaribisha na
kuzungumza na vyombo vya habari, leo Jijini Dar Es Salaam.
Mwezi Mei tarehe 9, mwaka 2015, Tanzania imeandika historia nyingine
baada ya kufanya Tiba ya moyo bila ya kufanya upasuaji kwa kuziba
matundu yaliyoko kwenye moyo kwa kutumia “kifaa maalum” bila kufungua
kifua kama ilivyozoeleka.
Tiba hii inafanyika kwa mara ya kwanza nchini kupitia Idara ya Tiba
na Upasuaji Moyo ya Hospitali ya Taifa Muhimbili ikishirikiana na
madaktari bingwa kutoka Hospitali ya Prince Sultan Cardiac Centre
iliyoko Riyadhi nchini Saudi Arabia ambao watakuwepo Muhimbili kwa siku
tisa kuanzia tarehe 9 hadi 16 Mei, mwaka huu.
Madaktari hawa wamekuja kupitia taasisi ya Al Mutanda Islami Trust ya
Uingereza. Akizungumza na wanahabari, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa
Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Hussein Kidanto amesema jumla ya
wagonjwa zaidi ya 20 wanatarajiwa kupatiwa tiba hii.
CHANZO: MICHUZI
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni