Kyoko Hamada katika mizunguko yake kama bibi kizee.
IMEZOELEKA kuwa binadamu wengi hupenda kuonekana vijana hata kama umri umeenda huku wengine wakitumia baadhi ya vipodozi, dawa za kuficha mvi na kuvaa mavazi yanayofanya waonekane vijana japo si vijana.
Mpigapicha Kyoko Hamada (42), yeye aliamua kuwa tofauti na kuishi kwa miaka miwili akijifanya bibi kizee ili kujua hasa wazee wanavyochukuliwa katika jamii.
Hamada, ambaye ni mzaliwa wa Tokyo, Japan aliamia nchini Marekani akiwa na miaka 15 na alipata wazo hilo baada ya kujitolea kutembelea makazi ya wazee wanaoishi maisha ya upweke.
Baada ya hapo aliamua kuanza mradi aliouita jina la 'I Used To Be You' ambapo alikuwa akizunguka mitaa ya New York kama bibi kizee na kupiga picha zake tangu mwaka 2012 na ameandaa kitabu cha picha chenye kurasa 99 ambacho atakichapisha.
Picha za Kyoko Hamada kabla na baada ya kujifanya bibi kizee.
Mama huyo anaeleza kuwa wakati mwingine watu walikuwa wakifungua
milango kwa ajili ya kumsaidia huku wengine wakimsaidia mizigo yake
mizito ila jambo la kushangaza alilojifunza ni kwamba hakuna mtu
aliyeonyesha kumjali au kumtambua.Baadhi ya picha za Hamda katika mradi wake huo:
na mwandish wetu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni