Maelfu ya raia wa Iraq wanaendelea
kuukimbia mji wa Ramadi huku kundi la wanamgambo wa Islamic State
likiwazuia na kuendeleza mashambulizi ya kuudhibiti mji wa Ramadi.
Umoja wa mataifa unasema kuwa watu elfu 25 wameutoroka mji huo katika siku kadhaa zilizopita, wakielekea mashariki hadi mjini Baghdad.
Raia wapatao elfu mia moja na thelathini walitoroka mji huo mwezi uliopita, ulipovamiwa na kundi la Islamic State.
Shirika la umoja wa mataifa pamoja na mashirika mengine, yameanza kusambaza chakula, maji na dawa, huku pia kambi za muda zikijengwa.
NA BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni