MTU mmoja aliyetambulika kwa jina la Abdikadiri Opapa anasakwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Temeke baada ya kumtorosha mtoto wa kambo na kumtishia maisha mke wake.
Akizungumza na mwandishi mwishoni mwa wiki iliyopita, Mwanaisha alidai kuwa mumewe huyo baada ya kumuiba na kumtorosha mtoto wake, amekuwa akimpa vitisho huku akisema pesa hizo zikicheleweshwa atamuua mtoto huyo.
“Mtoto aliyemtorosha sikuzaa naye alimkuta lakini wakati ananioa nilimwambia na akaniambia kuwa yeye ni mtu wa swala tano, hivyo nisiwe na wasiwasi naye,” alidai Mwanaisha.
Hata hivyo, alidai kuwa baada ya muda mwanaume huyo alibadilika akawa anampiga kila anaporudi nyumbani akiwa amekunywa pombe, hali ambayo alisema ilimchosha.Alisema baada ya kuona hali ya vitisho inazidi alikwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi cha Kizuiani, Mbagala na kufunguliwa jalada namba MBL/3345/2015 - KUTISHIA KUUA KWA MTANDAO.
Kuhusu kutoroshwa kwa mtoto wake amefunguliwa jalada namba MBL/RB/3200 / 2015- KUMTOROSHA MTOTO. Hata hivyo, wakati tunakwenda mitamboni imeelezwa kuwa mtoto huyo alikutwa kwa baba huyo wa kambo maeneo ya Manzese lakini bwana huyo hakupatikana hivyo anasakwa na polisi.
Stori: Haruni Sanchawa
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni