Huku nusu ya matokeo katika uchaguzi
wa rais nchini Nigeria yakiwa yametangazwa, mgombea kutoka chama kikuu
cha upinzani, Muhammadu Buhari, anaongoza dhidi ya rais aliye
madarakani, Goodluck Jonathan.
Tume ya uchaguzi imesema itaendelea kutangaza matokeo ya uchaguzi Jumanne asubuhi na kwamba matokeo ya mwisho yanatarajiwa kutolewa baadaye siku hiyo. Mwandishi wa BBC anasema yeyote atakayeshinda, litakuwa jambo la kushangaza iwapo mgombea atakayeshindwa hatatamka kuwepo kwa mbinu chafu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni