Baadhi ya wateja wa nguo wakichagua nguo kwenye soko la Mchikichini jijini Dar es Salaam.
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Miongoni mwa mambo ya aibu katika
jamii ni pamoja na masuala ya udhalilishaji wa kijinsia ukiwemo ule wa
maungoni hasa kwa wanawake.
Kwa muda mrefu mtandao huu umekuwa ukifuatilia vitendo hivyo vibaya
kwa jamii vinavyofanywa na watu waliokosa ustaarabu hasa jamii ya vijana
katika maeneo ya mikusanyiko ya watu wengi karibu maeneo mengi ikiwemo
jiji la Dar es Salaam.Miongoni mwa eneo linaloongoza kwa kuwadhalilisha
wanawake ni eneo la soko la Mchikichini lililopo Ilala Mkoa wa Dar es
Salaam.
Mtandao huu umekuwa ukishuhudia vitendo hivyo vibaya kwa jamii ambapo
wengi wa vijana wamekuwa wakifanya kwa makusudi kuwadhalilisha wanawake
hasa wasichana wadogo kwa kuwashika maungoni (makalio, kifua/maziwa)
huku wakiwalazimisha kununua bidhaa zao.
Vitendo hivi vimekuwa ni kama mchezo wa kawaida kwani vijana hao
wamekuwa wakiendeleza hali hiyo kwa muda mrefu sasa huku
wasichana/wakike hao wanaofanyiwa vitendo hivyo wakiwa hawana wa la
kufanya, Mtandao huu tunasema huo ni udhalilishaji na unatakiwa
kuchukuliwa hatua za haraka kukomeshwa kwani unakiuka maadili na utu wa
mwanamke.
tunatambua ipo mamlaka husika zinazoweza kulichukulia hatua suala
hili basi kama zipo zianze sasa kwani udhalilishaji huu huko mbele
unaweza kuleta madhara makubwa kwa mtendewa na hata anayetenda kwani
akiachwa sasa baadae anaweza kufanya tukio kubwa na likafumbiwa macho
ikiwemo kubaka.
Nachelea kuamini kama vijana hawa wanafanya hivi kwa kujiamini ama
kuna nguvu ya msukumo nyuma yake? Kipindi cha nyuma sote tumekuwa
tukishuhudia vijana hao wakiwachania nguo wanawake waliokuwa wakivaa
vimini waliokuwa wakipita katikati ya mitaa ya Kariakoo wakati huo huo
wamesahau kuwa nguo hizo wamewauzia wao, tukiacha hilo pia wapo hawa
Makondakta wa daladala nao ni miongoni mwa watu wanaoongoza kufanya
vitendo vya kidhalilishaji wanawake.
Mtandao huu umeweza kuliona hilo kwa upande wa Makondakta wa Daladala
nyingi hasa nyakati za abiria wa kike anapopanda hatua ya kwanza wao
wanapeleka mkono kwenye ‘Makalio’ ya Mwanamke na kumvutia ndani ya
daladala, yaani kama sapoti ya kumuingiza ndani.
Kondakta anafanya hivyo wakati huo amekaa mlangoni mwa daladala yake,
lakini anapopanda mwanaume usogea ndani ama hushuka chini bila hata ya
kumshika, lakini akipanda Mwanamke tu utakuta Konda anamshika makalio
kuona kwamba ni jambo la kawaida, Hivyo ni wakati sasa wa kubadilika
jamani vitu vingine hivi ni kushusha utu wa mwanamke hivyo tubadilike na
tuchukue hatua, Asante.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni