Idara ya usalama nchini Brazil imesema kuwa imewaua watu saba waliokuwa
wakifanya jaribio la kupora katika benk moja na ambao pia wanadaiwa
kujiusisha na dawa za kulevya.
Taarifa hizo zinasema kuwa majambazi hao walianza kurushiana risasi na
Polisi katika mji wa Novos Kaskazin Mashariki mwa Brazil.\
Mtu mmoja
anashikiliwa na Polisi,ambapo pia bunduki na vifaa vya milipuko
vilivyokuwa vinamilikiwa na watu hao vinashikiliwa. Katika tukio jingine
pia Polisi wamewaua watu wengine wanne wanaodaiwa kujihusisha na
biashara ya dawa za kulevya katika mji wa Rio de Janeiro.
Kuuawa kwa
majambazi hao kunafuatia mapambano ya polisi na kundi hilo,ambapo mabomu
na Bunduki vilikamatwa pia
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni