Dar es Salaam. Hatimaye leo wabunge wote wa vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wanakutana na viongozi wao wa jijini
hapa kumchagua mgombea urais atakayeviwakilisha vyama hivyo katika
Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Mkutano huo wa wabunge umekuja baada ya vikao
kufanyika mfululizo wiki hii, huku kukiwa na mvutano kuhusu nani au
chama gani kisimamishe mgombea urais.
Jana ililiripoti kwa uhakika habari zilizotoka ndani
ya vikao hivyo na kuthibitishwa na Mwenyekiti mwenza wa Ukawa, Dk
Emmanuel Makaidi, kuwa vyama hivyo vitaweka wazi mgombea wake wa urais
leo.
“Tumeshakubaliana namna ya kugawana kata na
majimbo 13 yaliyobaki na Jumamosi tutaweka wazi kwa wananchi. Pamoja na
hilo pia tutamtangaza mgombea urais na chama anachotoka,” alisema Dk
Makaidi.
Umoja huo umekuwa ukiongezeka nguvu tangu wakati
wa mchakato wa Katiba mwaka jana, hali inayosababisha wafuasi wake
kuamini kuwa yeyote atakayesimamishwa na umoja huo na kupigiwa kampeni
kwa pamoja anaweza kujikuta anakuwa rais, mbunge au diwani.
Mvutano
Vikao vya umoja huo vilitawaliwa na mvutano baina
ya wajumbe ndani ya umoja huo hasa katika nafasi ya mgombea urais baada
ya kuwapo kwa watia nia zaidi ya mmoja.
Chanzo cha uhakika kutoka ndani ya umoja huo
kilisema kuwa isingekuwa rahisi vikao vya namna hiyo vikakosa mvutano
huo, kutokana na baadhi ya wajumbe kushindwa kukubaliana na vigezo
vilivyowekwa tangu mikutano ya awali.
Iliilazimu Kamati Kuu ya Ukawa kufanya kazi ya
ziada kuhakikisha kuwa maridhiano yanafikiwa ili kumpata mgombea, ndipo
ikaamuliwa waalikwe wabunge wote wapige kura kupata mgombea.
Taarifa zaidi zilisema kuwa wajumbe walio wengi
walikuwa wanaipa nguvu Chadema kutoa mgombea urais kutokana na nguvu
yake hasa katika mikoa ya Bara, na ukweli kwamba tayari CUF
imekwishapewa fursa hiyo Zanzibar.
vyanzo vya ndani ya
kikao hicho, liliripoti kuwa licha ya kutangaza kugawana kata na majimbo
yaliyobaki, jina la mgombea urais lingetangazwa leo endapo wajumbe wa
Kamati Kuu ya Ukawa iliyokutana jana wangeafikiana.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha Azam jana,
Mbunge wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa alisema leo vyama hivyo
vitalitangazia dunia chama kipi kitatoa mgombea wa Ukawa.
na mwandishi wetu
na mwandishi wetu
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni