MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Ijumaa, 17 Julai 2015

Obama kutozuru kijiji cha babaake Kenya

                                                                        Barack Obama

ObamainKenya ndilo neno linalotawala mitandao ya kijamii nchini Kenya huku rais huyo akitarajiwa kulitembelea taifa hilo.
Hatahivyo wakaazi wa kijiji cha Kogelo ambapo babaake Obama alizaliwa na kulelewa sasa hawatalazimika kufanya maandalizi ya aina yoyote kufuatia ziara hiyo baada ya balozi wa Marekani nchini Kenya Robert Godec kusema kuwa rais huyo hatozuru kijiji cha Kogelo.
''Ana mda mchache sana kwa hivyo basi atakuwa nairobi pekee'',alisema bwana Godec akizungumza na runinga ya KTN.
Bibiye Obama Sarah Obama alikuwa amejiunga na wakaazi wa Kogelo akimtaka Obama kuwatembelea kulingana na ripoti za kituo cha habari cha Capital fm.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni