MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumatano, 1 Julai 2015

33 warudisha fomu urais CCM.



Wakati leo ikiwa ni siku ya mwisho ya kupokea fomu za wagombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wanaoo---mba kuteuliwa na Chama cha Mapinduzi (CCM) kugombea kiti hicho katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu; wagombea 33 pekee ndiyo waliorejesha fomu hadi kufikia jana jioni huku wagombea tisa wakiwa bado.
 
CCM ilifungua pazia kwa makada wake kuanza kuchukua fomu za kuomba kuteuliwa kugombea kiti cha urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Juni 3, mwaka huu.
 
Wagombea ambao hawajarejesha fomu mpaka sasa, ni Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba, Mbunge wa Sengerema, William Ngeleja, Ritha Ngowi, Hellena Dina Elinawinga, Anthony Chalamila, Banda Sonoko, Peter Nyalali na Mussa Mwapango.
 
Hata hivyo, Naibu Katibu Mkuu (Bara) wa CCM, Rajab Luhwavi, alisema kuwa wagombea tisa ambao hawajarejesha fomu hiyo, watapaswa kuzikabidhi kabla ya muda wa mwisho wa kupokea fomu za wagombea urais kufungwa rasmi leo saa 10:30 jioni.
 
“Mpaka sasa tumepokea fomu za wagombea wa urais 33 kati ya 42 waliochukua fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama kugombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 2015. Muda wa mwisho kupokea fomu hizo kwa waliobaki ni kesho (leo) saa 10:30 jioni, tutakapochora mstari wa mwisho,” alisema Luhwavi.
 
Baada ya kukamilika kwa kazi ya urejeshaji wa fomu, makada hao 42 watasubiri kufanyika kwa vikao vya juu vya maamuzi.
 
Vikao hivyo ni pamoja na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa itakayokutana Julai 7 na Kamati Kuu (CC) itakayokutana Julai 8, chini ya Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Jakaya Kikwete, ikifuatiwa na kikao cha Nec Julai 9, mwaka huu.
 
Mchakato wa kumpata mgombea urais atakayepeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu, utahitimishwa Julai 11, mwaka huu na Mkutano Mkuu wa Taifa CCM ambao ni maalum kwa ajili kulipigia kura jina la mgombea mmoja kati ya watatu. 
CHANZO NIPASHE

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni