MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumatano, 1 Julai 2015

Libya kuunda serikali ya Umoja?

Wa                           ziri Mkuu wa Serikali ya Libya inayotambuliwa, Abdullah al-Thinni

Kiongozi wa serikali ya Libya inayotambuliwa kimataifa, Abdullah al-Thinni amesema ana matumaini ya kutia saini ya makubaliano ya kugawana madaraka na wapinzani wake wa kisiasa.
Al-Thini amesema ana matumaini ya kufikiwa makubaliano katika awamu nyingine ya mazungumzo ya amani yatakayofanyika nchini Morocco siku ya Ijumaa.
Hali ya usalama nchini Libya imekuwa tete tangu wanamgambo walipoudhibiti mji mkuu wa nchi hiyo,Tripoli, mwaka jana na kuweka Bunge lao.
Al-Thini ni Waziri mkuu katika Serikali iliyoweka makao yake katika eneo la mashariki ya mji wa Tobruk.
Mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini humo amekuwa akifanya jitihada za kuhakikisha kuwa pande hizo mbili hasimu zinaunda Serikali ya umoja wa kitaifa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni