Shirika la Kimataifa la Biashara Duniani, WTO limesema India haijafanya uamuzi wa haki kuzuia uingizaji wa kuku na mayai kutoka Marekani kwa hofu ya ugonjwa wa mafua ya ndege.
Shirika hilo linaendelea kushikilia uamuzi uliotolewa katika mahakama ya usuluhishi wa masuala ya kibiashara uliofanyika Oktoba mwaka jana. India iliweka vikwazo vya kibiashara tangu mwaka 2007, ikisema inataka kuzuia mafua ya ndege kuingia katika nchi yake. Ingawa WTO inasema sheria zilizowekwa na India hazikufuata viwango vya kisayansi vya kimataifa.
Uongozi wa serikali ya Rais Obama umekubaliana na uamuzi huo, ingawa kiwanda cha kuku nchini Marekani kimeona kuwa India inaacha kupokea kuku wenye thamani ya dola milioni mia tatu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni