Ugiriki imetangaza kuchelewa kulipa deni la Euro milioni mia tatu ambalo walitakiwa kulilipa shirika la kimataifa la fedha la IMF siku ya Ijumaa.
Serikali ya Ugiriki imesema itachanganya kwa pamoja malipo hayo ambayo yalikuwa yalipwe kwa mafungu manne mwezi June ya kuyalipa kwa pamoja mwishoni mwa mwezi huu.
Utaratibu huo ambao unaruhusiwa na kanuni za IMF,uliwahi kufanywa na nchi ya Zambia miongo mitatu iliyopita.
Mwandishi anasema mpango huo unaweza kuwa mbinu ambayo Ugiriki umeitumia ili kuweka msisitizo kwa wadeni wake wa kimataifa wakati huu nchi hiyo ikitafuta ufumbuzi wa madeni yanayolikumba taifa hilo.
NA BBC
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni