NAIBU Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Makamba ambaye ni mmoja wa makada wa CCM waliotangaza nia ya kuwania kuteuliwa kuwania Urais, ameibuka na ubunifu wa kisasa katika namna ya kutangaza nia ya kuwania urais kupitia CCM, kitu ambacho endapo kitafanikiwa atakuwa amemfunika Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa ambaye kwa sasa ndiye gumzo miongoni mwa makada waliojitokeza.
Edward Lowassa. |
Januari, ambaye ni mtoto wa Katibu Mkuu wa zamani wa CCM, mzee Yussuf Makamba, jana katika Ukumbi wa Mlimani City, alitegemewa kutangaza nia ya kutaka nafasi hiyo ya juu kisiasa nchini, katika tukio ambalo lingeonekana pia katika kumbi mbalimbali nchi nzima zilizokuwa zimeandaliwa na kujaza watu waliomsikiliza na kuuliza maswali ya moja kwa moja.
Januari Makamba |
Akizungumzia kuhusu suala hilo, Makamba alisema kumbi katika mikoa mbalimbali nchini zilikuwa zimeandaliwa, ambazo zingefungwa skrini kubwa ambayo watu waliomo wangeweza kumuuliza maswali Makamba akiwa Mlimani City jijini Dar es Salaam, teknolojia ambayo itakuwa inatumiwa kwa mara ya kwanza na mwanasiasa nchini tangu Tanzania ipate uhuru wake.
Licha ya kuonekana katika skrini hizo, watu wangepa fursa ya kuuliza maswali na kujibiwa papo kwa papo kutoka popote walipo.
Kabla ya ubunifu huo, Lowassa alikuwa akishikilia rekodi ya tukio lake la kutangaza nia kwa kujaza watu wengi uwanjani huku maelfu wakifuatilia katika vituo vya televisheni tukio hilo lililofanyika Mei 30, jijini Arusha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni