Serikali imetekeleza ahadi ya Rais Jakaya Kikwete ya kujenga Barabara kutoka Kyaka hadi Kasulu mkoani Kigoma kwa asilimia 80.
Mhandisi wa Barabara hiyo, Mushubila Kamundwa, alimueleza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, alipotembelea na kukagua barabara hiyo ambayo ina urefu wa kilometa 176.
Alisema barabara hiyo iliyogharimu Sh. Bilioni 65, inaratajiwa kukamilika mwezi Desemba, mwaka huu.
Alitaja changamoto zinazowakabili ni fedha za kuwalipa wakandarasi na Shirika la Umeme nchini (Tanesco), kuchelewa kutoa miundombinu yao barabarani.
Kinana aliahidi kuzungumza na Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, ili kuona namna ambavyo fedha za kuwalipa na kumalizia kazi hiyo itakavyopatikana.
Alifafanua pia kuwa, ujenzi huo ni sehemu ya miradi mingi aliyoahidi Rais Kikwete alipotaka kuingia madarakani mwaka 2010 na kwamba utekelezaji upo kwenye hatua za mwisho.
NA MARY GEOFREY
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni