MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumanne, 16 Juni 2015

Mwili wa marehem Mufti Simba wawasili Shinyanga


MWILI WA MARSheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti, Issa Shaaban Bin Simba amefariki dunia jana katika Hospitali ya TMJ, Dar es Salaam alikokuwa amelazwa akisumbuliwa na shinikizo la damu na kisukari.
siku ya leo majira uya saa nane mchana mwili wa marehem sheik simba umewasili shinyanga kwajili ya taratibu za mazishi


NSerikali, viongozi watuma salamu za rambirambi
Rais Jakaya Kikwete ametuma salamu za rambirambi kwa Waislamu wote nchini na Bakwata kutokana na kifo hicho.
“Kifo kinaleta huzuni. Hata hivyo, hakizuiliki, hatuna budi kukikubali na ni wajibu wetu kumuombea Sheikh Mkuu kwa Mola wetu ampe mapumziko ya milele,” ilisema sehemu ya salam hizo za Rais Kikwete alizotuma kupitia kwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum.
“Nawaombea subira wana familia, ndugu, jamaa, Waislamu wote na wanajamii kwani Mufti alikuwa kiongozi katika jamii yetu. Kamwe mchango wake hautasahaulika katika jamii yote kwa ujumla na hakika sote tutamkumbuka,” alisema Rais.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni