MMILIKI WA BLOG HII

MMILIKI WA BLOG HII
TANGAZA NASI MATANGAZO YA KIJAMII BURE KUPITIA BLOG HII

Jumanne, 16 Februari 2016

DC AMFUKUZA KAZI MEO SOMANDA KWA WIZI WA CHAKULA CHA MSAADA


CHAKULA CHA MSAADA KINAVYOWANUFAISHA VIONGOZI

MKUU wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu,Paunsiano Nyami amemsimamisha kazi Mtendaji wa kata ya Somanda wilayani hapo,Joseph Shabalanga kwa kosa la kutorosha gunia 6 za mahindi ya msaada katika ngala la chakula hicho.

Alieleza kuwa Mtendaji huyo,alitokomea kusiko julikana baada ya chakula hicho kukamatwa mpaka Mkuu huyo wa wilaya alipoamua kutumia lugha za kumshawishi kuwa hawezi kuwa na hatia kwa njia ya simu hali ailiomsababisha mtendaji huyo ajisalimishe kwa jeshi la polisi.

Akizungumza Nyami alisema mnamo tarehe 11 february magunia 6 ya mahindi yalitorosha na watu wasiojulikana pasipo kujua ni njia gani zilitumika kutorosha chakula hicho kIsha February 12 majira ya saa 6 usiku baadhi ya magunia 6 ya chakula hicho yalishikwa maeneo ya Somanda Mkoani hapo.

Nyami akiyabainisha yaho juzi ofisini kwake alisema kuwa jeshi la polisi  wilayani hapo liliwakamata wenyeviti wa mitaa kata ya somanda  kwajili ya upelelezi huku wakiwawameweka ndani mlinzi wa mahakama ya somanda,Sitta Burugu,Anna Shushi mtendaji wa kata ya Nyaumata na Salome Masalila mtendaji wa mtaa Somanda.


NA MWANDISHI WETU

“Mh waziri jenista alifofika kuangalia hali ya njaa katika Mkoa wetu aliahidi kuleta chakula mapema na baada ya muda kweli kilifika.chakula hiki kilikuwa ni kwajili ya watu ambao hawajiwezi kabisa..wale maskini ambao hawajiwezi kwa kila kitu ndio ambao tunawapatia chakula hiki”Alisema.

“Mtazamo wa suala hili ni wizi tumejaribu kumtafuta aliyeuziwa magunia hayo 6,mpaka sasa bado hajaoneka ila tumemtambua ni mfanyabiashara wa duka maeneo ya somanda anaitwa,Shulinde”Aliongeza.
Aidha alisema kuwa katika halmashauri ya wilaya Bariadi walipokea tani 70 nahalmashauri ya Mji ikipokea tani 51.01 kwajiri ya chakula hicho cha msaada.

Alisema watendaji wa mitaa 10 wilayani hapo wamejipanga kutoa elimu kwa wananchi ili wajue ni watu gani ambao wanastahili kupata chakula hicho


Sambamba na hayo Nyami ametoa wito kwa viongozi waliochaguliwa na wanachi kuwa waadilifu katika kazi kwa kuzingatia sheria na kwa watakao kiuka taratibu hatasita kuwachukulia hatua za kisheria.


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni